Meneja wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema Kiungo Mshambuliaji Eden Hazard yupo kwenye mipango ya klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujayo.

Ancelotti ametoa msisitizo huo, huku kiungo huyo kutoka nchini Ubelgiji akionyesha dalili za kurejea katika kiwango chake.

Mpaka sasa Hazard mwenye umri wa miaka 31, amehusika kwenye mabao ya Real Madrid katika michezo miwili iliyopita na amekuwa akianza kwenye kikosi hicho.

“Ndio, yupo kwenye mipango kwa msimu ujao,” amesema kocha huyo kutoka nchini Italia.

Hazard ameripotiwa kukataa kuondoka klabuni hapo mwezi huu, akikataa ofa ya klabu ya Newcastle United.

Try Again: Ubingwa Tanzania Bara bado sana
Young Africans yarejea Dar es salaam