Kikosi cha Young Africans kimerejea jijini Dar es salaam kikitokea Jijini Arusha, baada ya kumaliza kazi ya kuiadhibu Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Mzunguuko wa 13 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Young Africans iliikabili Polisi Tanzania jana Jumapili (Januari 23) kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kuibuka na ushindi 1-0, lililofungwa na Dickson Ambundo akiunganisha pasi ya Mshambuliaji Fiston Mayele.

Kikosi cha vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kimewasili Dar es salaam kwa ndege ya shirika na ndege la Tanzania (Air Tanzania).

Ushindi dhidi ya Polisi Tanzania umeiwezesha Young Africans kufikisha alama 35 zinazoendelea kuiweka kileleni, wakiwaacha Mabingwa watetezi Simba SC kwa tofauti ya alama 10.

Simba SC ipo nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 25, huku ikicheza michezo 12, ikidaiwa mchezo mmoja wa kiporo dhidi ya Kagera Sugar ili kuwa sawa na Young Africans.

Young Africans itacheza tena mwishoni mwa juma hili mchezo wa hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Mbao FC kutoka Jijini Mwanza.

Eden Hazard kupeta Real Madrid
Mume, mke washikiliwa kwa makosa ya mauaji