Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen amewaacha wachezaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Wakongwe John Bocco na Erasto Nyoni.

Kocha Poulsen leo Jumanne (Machi 15) ametaja kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza michezo ya Kimataifa ya Kirafiki iliyo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa ‘FIFA’ juma lijalo.

Michezo hiyo ya Kimataifa ya Kirafiki inalenga kuiandaa Stars kwenye Mshike Mshike wa kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2023 ‘AFCON’ na Fainali za Mataifa Bingwa Afrika 2024 ‘CHAN’

Kocha huyo kutoka nchini Denmark amesema wachezaji hao wakongwe bado wana nafasi ya kurudi kwenye kikosi cha Taifa Stars katika kipindi hiki cha maandalizi ya michezo hiyo ya Kimataifa ya Kirafiki, hivyo wana kazi ya kufanya ili kumshawishi.

“Erasto na Bocco hawatokuwepo lakini bado wana nafasi ya kurejea wakati tukiwa kambini na bado kuna muda kabla ya kucheza michezo yetu” amesema Kim Poulsen

Bocco na Erasto wamekua na wakati mgumu wa kuanza kwenye kikosi cha Simba SC tangu kuanz akwa msimu huu 2021/22, na huenda hiyo imekua sababu ya kuachwa kwao kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Wakati wachezaji hao wakongwe wakiachwa, wachezaji wa Simba SC waliotajwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Mohamed Hussein, Mzamiru Yassin, Jonas Mkude na Kibu Denis.

Wachezaji wa Young Africans waliotwa Taifa Stars ni Abutwalib Mshery, Bakari Nondo Mwamnyeto, Farid Mussa, Zawad Mauya na Feisal Salum.

Wachezjai wengine ni Metacha Mnata (Polisi Tanzania), Haji Mnoga (Weymouth ya Uingereza), Lusajo Mwaikenda wa Azam FC), Abdulrazack Hamza (Namungo), Nickson Kibabage (KMC FC), Novatus Dismas (Beltar Tel Aviv Bat Yam ya Isarel), Aziz Andambwile (Mbeya City), Simon Msuva (Wydad ya Morocco), Kelvin John (Genk ya Ubelgiji), Ben Starkie (Spalding ya Uingereza) Mbwana Samatta (Antwerp ya Ubelgiji), Tepsi Evance wa (Azam FC), Relliats Lusajo wa (Namungo), George Mpole (Geita Gold) na Ibrahim Joshua (Tusker ya Kenya).

Simba SC yatamani kumaliza kinara Kundi D
Kiiza: Kuifunga Simba SC kumeniponza