Mkazi wa Kijiji cha Sibwesa wilayani Tanganyika, Mande Emanuel (30) amejinyonga baada ya kumjeruhi mumewe, Dotto Enos (35) kwa kumkata mapanga.

Akizungumza na Dar24Media leo Machi 20, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliosababishwa na shughuli za kilimo.

Katika hatua nyingine Kamanda Makame amesema katika kijiji cha Kapanga wilayani Tanganyika amemkamatwa Julias Lyamkolo {63) akiwa na bangi gramu 250.

Aidha mtuhumiwa huyo amekiri kuwa yeye ni mkulima wa bangi na aliwapeleka polisi kuwaonyesha shamba lenye ukubwa wa ekari 4 alilopanda mahindi na bangi.

Rais Museveni atangaza kifo cha Spika wa bunge
Bwawa la Chamakweza kufanyiwa marekebisho