Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza kifo cha spika wa Bunge la Uganda acob Oulanyah ambaye amefariki dunia akiwa nchini Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah amefariki dunia nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Rais Museveni ametangaza kifo cha spika huyo kupitia akaunti yake ya Twitter.

Katika ujumbe wake aliotaangaza kifo hicho, Rais Mseveni amemtaja Oulanyah kama kada mzuri.

Hakuweka wazi kilichosababisha kifo cha Spika huyo ambaye alikuwa amelazwa hospitali nchini Marekani kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Oulanyah aliingia kwenye nafasi hiyo Mei 2021 na kabla ya kuwa Spika alikuwa naibu Spika kuanzia 2011.

Oulanyah mwanasheria na mwanasiasa wa muda mrefu aliwahi kuwa mbunge wa Kaunti ya Omoro, Kaskazini mwa Uganda.

Oulanyah alikuwa miongoni mwa wanasiasa kutoka eneo hilo walioshiriki katika mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Uganda na waasi wa Lord’s Resistance Army walioongozwa na Joseph Kony miaka ya 2000.

Sakata la Fastjet na wafanyakazi wake laibuka upya
Ajinyonga baada ya kumkata mumewe na mapanga