Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza kifo cha Faru Rajabu kilichotokea usiku wa kuamkia leo katika hifadhi ya Serengeti.

Faru Rajabu amefariki akiwa na umri wa miaka 43 na sababu za kifo chake zimetokana na Uzee ambapo wastani wa maisha ya Faru weusi ni kuaniza mika 35 hadi 40.

TANAPA imesema kuwa mwili wa faru Rajabu utahifadhiwa kwa namna ambayo inaendana na kanuni za Asili za Uhifadhi.

Faru Rajabu alizaliwa mwaka 1979 katika hifadhi ya Ngorongoro na kuhamia hifadhi ya Serengeti mwaka 1993 na alikuwa na watoto, wajukuu, na vitukuu.

Barbara: Hatupaswi kupoteza lengo letu
Kenya: Wagombea Urais wajiengua