Serikali ya Taliban imeamuru mashirika ya ndege nchini Afghanistan kuwazuia wanawake kupanda ndege bila kuongozana na jamaa yeyote wa kiume.
Maafisa wa anga wa Taliban wamealiambia shirika la habari la AFP Sheria hiyo kali inafuatia kufungwa kwa shule zote za sekondari za wasichana saa chache baada ya kuruhusiwa kufunguliwa tena kwa mara ya kwanza tangu wapiganaji hao wa Kiislamu wenye misimamo mikali kuchukua mamlaka mnamo Agosti 2021.
Maafisa wawili kutoka shirika la ndege la Ariana Afghan la Afghanistan na Kam Air, wamesema sheria hiyo iliwekwa siku ya Jumapili, Machi 27 jioni, wakati Taliban wakiamuru mashirika hayo kutoruhusu wanawake kuabiri ndege wakiwa wanasafiri pekee yao.
Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya mkutano wa Alhamisi kati ya wawakilishi wa Taliban, mashirika mawili ya ndege na mamlaka ya uhamiaji wa viwanja vya ndege.
Tangu kurejea kwa Taliban madarakani, Sheria kali dhidi ya wanawake, vikwazo vingi vya uhuru wa wanawake vimerejeshwa, Wanawake wamebanwa nje ya kazi nyingi za serikali na elimu ya shule ya upili, na pia kuamriwa kuvaa kulingana na tafsiri ya Kurani.
Maelfu ya wasichana walimiminika tena darasani Jumatano baada ya shule kufunguliwa, lakini maafisa waliwaamuru warudi nyumbani saa chache kabla ya siku hiyo, na kuzua hasira ya kimataifa.
Mnamo Septemba 2021, wanawake walioajiriwa na serikali jijini Kabul walizuiliwa kufanya kazi hadi watakaposhauriwa kufanya hivyo, Isitoshe, wanafunzi wa kike katika vyuo vikuu walitenganshwa na wa kiume ili kuzingatia sheria za kiislamu kuhusu mavazi.
.