Rais wa FC Barcelona Joan Laporta amesema hafahamu kama Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Ousmane Dembele atabaki klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Laporta amekua mstari wa mbele kuhakikisha Dembele anabaki klabuni hapo, kwa kuanzia mazuingumzo ya kumsainisha mkataba mpya, kufuatia mkataba wa sasa kufikia kikomo mwezi Juni.

Hata hivyo, Makamu wa Rais wa FC Barcelona Rafael Yuste amesema: “Ikiwa Dembele ataendelea kujisikia vizuri, basi tunaweza kukutana na mawakala wake na anaweza kubaki.”

Rais wa Barca Laporta amesema hakuna mabadiliko yoyote kuhusu mustakabali wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Borussia Dortmund, huku miamba hao wa Catalunya wakijitahidi kupigania ubingwa wa LaLiga baada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 wa Clasico dhidi ya Real Madrid.

Kiongozi huyo ameliambia gazeti la Mundo Deportivo: “Dembele ni mvulana mzuri na wa aina yake, angalau hajatuletea matatizo tangu tulipoiongoza klabu.

“Labda tunamwona Dembele bora tangu akiwa Barca, hakika ni mchezaji ambaye makocha wanamfahamu vema zaidi, kuanzia Xavi ambaye anamsimamia vizuri mchezaji huyo.

“Lakini tulimpa ofa ya kumwongeza tena mkataba ambayo uliisha Desemba 20 mwaka jana. Aliamua kutotumia fursa. Sasa Xavi amesema alikuwa akimtegemea kwa sababu ni mchezaji anayeleta mabadiliko.

“Sasa kuongezwa upya kwa Dembele? Ngoja tuone chaguo alilokuwa nalo limeisha na tayari tunapanga viwango vya mishahara ambavyo wale wote watakaosalia msimu ujao watalazimika kuvikubali. Viwango vingine vinapaswa kudumisha uendelevu na uwiano wa klabu na kikosi.”

Alipoulizwa kama Barca watatoa ofa mpya kwa Dembele, Laporta alijibu: “Kwa sasa, kwa madhumuni yetu, hatuna habari kwamba anataka kuendelea.

“Sijui kama mwakilishi wake amekuwa akiwasiliana, lakini nadhani si kwa sababu angejua na kimsingi tunazingatia hatua hii ya mwisho ya ligi kujaribu kufanya makubwa na kushinda.

“Mwisho wa msimu, nadhani kwa namna fulani kutakuwa na mazungumzo lakini ndani ya viwango vya mishahara ambavyo tunaanzisha.”

Kiungo chipukizi Gavi na mlinzi wa Uruguay, Araujo wana mkataba na Barca hadi mwisho mwa msimu ujao, lakini Laporta hana wasiwasi wowote kuhusu mustakabali wao.

Amesema: “Hii iko kwenye njia sahihi. Ndio, ni wachezaji ambao tunataka kuendelea nao, ndani ya viwango hivi vya mishahara tunayoanzisha. Tungependa waendelee kwa miaka mingi.”

Wanawake marufuku kusafiri bila kuandamana na mwanaume
Profesa Ngowi afariki Dunia