Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Anna Makinda amewataka jamii za wafugaji kuhakikisha siku ya sensa wanakuwepo katika maeneo yao ili waweze kuhesabiwa huku akiisihi jamii kuhakikisha makundi maalum nayo yanashirikishwa katika zoezi hilo bila kificho.

Anna Makinda ambae ni kamisaa wa Sensa nchini ametoa rai hiyo wakati wa semina ya uhamasishaji viongozi wa kidini na mila iliyoandaliwa na taasisi ya dini ya TWARIQA TUL QADIRIAYA JAILAN YA ARRAZQIA ya jijinj Arusha

Aidha amewaomba viongozi hao kuhakikisha wanatoa elimu na kuwahamasiha wananchi na waumin wao umuhimu wa kushiriki katika zoezi hilo ili liweze kufanikiwa na kusaidia nchi kupanga mipango yake.

Katibu mkuu wa taasisi ya TWARIQA Yahaya Mkindi amesema taasisi hiyo ipo tayari kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali ambapo kwa kutambua umuhimu wa sensa wamechukua jukumu la kuelimisha jamii kwa makundi mbalimbali.

Serikali ya Tanzania ipo kwenye maandalizi ya kufanya sensa ya makazi na watu inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti sensa ambayo itakuwaaa ya sita tangu nchi ipate uhuru.

Tanzania na Liechtenstein kuwekeza kwenye kilimo
Msemaji Mkuu wa Serikali ameipongeza Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro