Mgombea urais nchini Kenya, na Makamu wa rais, William Ruto amepuuzia taarifa kuwa alijaribu kupindua serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.

William Ruto amekanusha madai kuwa alipanga kupindua serikali akizungumza Mombasa katika muendelezo wa kampeni za uchaguzi jana Jumapili machi 27 akisema yeye ndiye alisaidia serikali ya Jubilee kuingia madarakani na hivyo hawezi kuipangia mabaya.

“Tafadhalini my friends, mkuwe na heshima kidogo. Mimi ndio nilisaidia Uhuru Kenyatta, hata kama hamtaki kuniunga mkono wacheni porojo na propaganda ya bure, wacheni kugawanya waKenya bure. Eti William Ruto anaweza kupindua mtu niliyemweka katika afisi?” alisema DP Ruto.

DP Ruto alisema taarifa hizo zimeandaliwa na baadhi ya watu ndani ya serikali kama njia ya kujaribu kumchafua wakati huu wa kampeni za uchaguzi

“Kwa sababu Wakenya wamekataa kupangwa na nyinyi, Wakenya wamekataa project yenu ambayo mnataka kutumia kuendesha ukimabavu juu yetu “Mimi ni mtu mzima, mimi si mlevi mimi si mwendawazimu eti niweke serikali ndani alafu niende nifanye njama eti kuipindua,” alisema DP Ruto.

Ruto aliongeza kuwa, “Mtu wa kupindua serikali ako Kenya hii na anajulikana. 1982 alikuweko akijaribu kupindua serikali, hivi majuzi si alijiapisha akijaribu kupindua serikali. Stop confusing me with your project,”

Alisema ripoti za kuipindua serikali zinaweza kuleta mgogoro wa kisiasa nchini huku akionya dhidi ya ripoti kama hizo, “Msilete porojo zisizo na amani. Kwa sababu hamna mpango ndio mnaleta huu upuzi, “Mimi kama naibu rais najua kazi yangu na sijawahi, sitawahi na sitawahi kuwa na njama ya kujaribu kuiangusha serikali ya Kenya. Shame on you!”alisema Ruto Jumapili Machi 27.

Uchaguzi wa Kenya unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti 2022, na mpaka sasa vinara wa uchaguzi huo ni Ambaye ni msaidizi wa Rais, William Ruto na Kiongozi wa chama cha Upinzani Raila Odinga.

Msemaji Mkuu wa Serikali ameipongeza Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro
Tiketi za kieletroniki kuanza Julai mosi