Wakala wa barabara za vijijini na Mijini imetoa taarifa kwa umma juu ya Faini ambazo zimekua zikitolewa kwa wamiliki wa magari kutokana na kutokulipa ushuru wa kuegesha magari.
Katika taarifa yake kwa umma TARURA imeeleza kuwa faini hizo zinaanza kulipishwa kuanzia siku 14 ambapo mmiliki anakua hajalipa Ushuru alioandikiwa.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kuanzia tarehe 7 Aprili 2022, faini hizo zimeanza kutumika rasmi baada ya kutoa muda wa kuwaelimisha wamiliki wa vyombo vya usafiri kuanzia tarehe 3 Disemba 2021 ambapo chapisho la serikali lilitoka kwa mara ya kwanza juu ya sheria ya maegesho ya magari.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa malipo ya faini yatatozwa kwa wamiliki waliochelewa kulipa kuanzia tarehe 1 Marchi 2022, na kila faini itajiongeza kutokana na deni la siku husika hadi kuhesabu siku 14 za deni.
Watumiaji wote wa magari wametakiwa kukumbuka kulipa deni la ushuru wa magari kwa wakati na kuhakikisha kila wakati kwa kupiga *152*00# na kuhakikisha hawana madeni ya maegesho.