Seneti ya Marekani imemthibitisha Mwanamke wa kwanza Mweusi kuhudumu katika nafasi ya Jaji wa mahakama kuu nchini Marekani.

Jaji Ketanji Brown Jackson anaingia katika dawati la timu ya watu Tisa katika historia ya mahakama hiyo kwa Miaka 233, na anachukua nafasi ya Jaji Stephen Breyer abbaye anastaafu mwezi juni mwaka huu.

Kura hiyo iliyosimamiwa na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris siku ya alhamis, imethibitisha uchaguzi wa Rais Biden ambaye alimteua Jaki Ketanji kwa kura 53-47, na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa jaji katika mahakama ya juu zaidi nchini humo.

Wakati kura hiyo ikiendelea, Rais Joe Biden na Jaji Ketanji Brown walikua wakifuatilia zoezi hilo kupitia ikulu ya ‘White House,’ Warepublican watatu Susan Collins, Lisa Murkowski na Mitt Romney wote walipiga kura kumuidhinisha jaji huyo mwenye umri wa miaka 51, jaji wa tatu pekee mweusi katika historia ya Mahakama ya Juu ya Marekani.

Jaji Ketanji hapo kabla alihudumu kama jaji wa Mahakama ya kazi ya Marekani ambapo aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Barrack Obama mwaka 2013, na kabla ya hapo alihudumu katika Tume ya Hukumu ya Marekani na kama Mtetezi wa jamii.

Wanademokrat walimsifu Jackson kwa uzoefu wake wa kina, alihudumu kama jaji kwa karibu miaka 10 katika ngazi ya serikali kuu na rufaa, na karani wa jaji wa Mahakama ya Juu Stephen Breyer, ambaye Rais Joe Biden amemteua kuchukua nafasi yake.

Katokana na mtandano wa NBS wa Marekani Inasemekana pia ukiachana kuweka utofauti wa kijinsia na asili ya Jaji Ketanji, Rais Biden pia alifikiria bora katika utendaji wa juu katika mahakama hiyo akiangalia zaidi watu ambao ni wanatetea jamii, wanaotetea haki za binaadamu na wąchache ambao ni wanasheria.

Moto tena Soko la Karume
UN yaiondoa Russia kwenye Baraza la haki za binadamu