Waziri wa Maji Juma Aweso amewachukulia hatua waliohusika na Ubadhilifu wa fedha millioni 600 zilizotengwa kwaajili ya kukamilisha mradi wa bwawa la maji la kata ya Kwemkambala Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga ambapo mradi huo mpaka sasa umeshindwa kutekelezeka
Waziri Aweso amechukua hatua hiyo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya mradi huo ambapo wahusika wameshindwa kutoa maelezo sahihi ya matumizi ya fedha hizo .
Aidha waziri huyo amewachukulia hatua waliohusika na ubadhilifu wa fedha hizo ambao ni mtaalamu wa mabwawa kutoka wizara ya maji, mthibiti ubora wa wizara hiyo pamoja na Mkandarasi wa mradi huo .
“Serikali inayoongozwa na Rais samia haiwezi kuvumilia uzembe wa aina hii mnasema fedha zimetumika kumlipa mkandarasi na hapa hakuna kazi inayoonekana ocd wachukue hao wakatoe maelezo sahihi”amesema wazir Aweso.
Waziri amesema fedha hizo zilipelekwa mahususi kwa wananchi wa eneo hilo waweze kupata maji safi na kuwaondolea adha hiyo ambayo inawabili tokea mwaka 2018 .
Awali akitoa malalamiko mbele ya Waziri diwani wa Kwedihamba Musa Abedi amesema wananchi wa eneo hilo walipisha mradi huo tokea mwaka 2019 mpaka leo hawapata maji na mashamba yao yalichukuliwa.
”Kama mkandarasi anaweza akalipwa Fedha zaidi ya milioni 300 na hajafanya chochote mpaka leo wananchi hawana maji kwanini wasilipwe fidia maana wengine walikuwa na mashamba yao eneo hilo”