Rais wa Marekani Joe Biden amevitaja vita vya Urusi nchini Ukraine kuwa mauaji ya halaiki, yanayolenga kuiangamiza Ukraine.

Akizungumza katika hafla moja huko Iowa, alipokuwa akielezea kupanda kwa gharama ya nishati kutokana na mzozo huo, Biden amesema kwamba Putin anatekeleza mauaji ya halaiki dhidi ya Ukraine.

Kauli ya Biden imepongezwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, ambaye amekuwa akiwahimiza viongozi wa magharibi kutumia neno hilo kuelezea uvamizi wa Urusi katika nchi yake.

Ukraine imekuwa ikiishutumu Urusi kwa kufanya uhalifu wa kivita, hata kabla ya kugunduliwa kwa miili ya watu wanaodaiwa kuuawa mjini Bucha.

Chini ya sheria za kimataifa, mauaji ya halaiki huchukuliwa kama dhamira ya kuharibu kwa ujumla au sehemu ya taifa, kabila, rangi au kikundi cha kidini.

Waziri Aweso achukizwa na matumizi mabaya ya mil. 600
Niliitwa mchawi kisa ndoto za kutembea