Ushindi wa Simba SC wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini umemuibua Haji Manara na kutoa neno katika furaha ya Wanamsimbazi ambao jana Jumapili (April 17) walishuhudia kandanda safi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Manara ameamka leo Jumatatu ya Pasaka (April 18) na kuandika ujumbe mrefu katika ukurasa wake wa Instagram akiipongeza Simba SC kwa ushindi huo huku akiwaita watani, na hii ni baada yay eye kuhamia upande wa Young Africans.
Mbali na kuwapongeza, Manara ameonyesha kuwa na shaka kuhusu kauli iliyotolewa na Kocha wa Orlando Pirates Mandla Ncikazi, ambayo ilidhirisha hakuridhishwa na maamuzi ya Penati huku akidai VAR uliyokua imefungwa Uwanja wa Mkapa haikutumika ipasavyo kutoa maamuzi sahihi ya mkwaju huo.
Manara ameandika: Kutoka Kaskazini hadi kusini mwa Afrika, tokea Mashariki hadi Magharibi mwa Bara hili adhimu, hata Ukija pale katikati ya Continent yetu, Kila mmoja analalamikia hilo hilo la udhalimu nje na ndani ya Uwanja.
May be wanawaonea gere, lakini why wote waseme hvyo hvyo? Au choyo kimewazidi?
Tufanye Kocha huyu kapata hasira za kufungwa, wale makocha wa vilabu vingine vilivyokuja hapa je?
Kama Mtanzania hayo hayakuhusu, as longer us Club ya nchi yako imeshinda, wewe ni kushangilia tu, wameshindaje ,hizo sio shida zako Mbongo.
But kama Mzalendo wa Afrika na muumini wa Fair game kwenye football, nje na ndani ya Pitch, kwa trend hii ya complains toka kwa clubs za wenzetu , na ikiwa ni mwendelezo ule ule,, unajisikiaje kila team ya nchi yako ikishinda,kuwe na Malalamiko yale yale?
Je Nchi kama Nchi haiwezi kupata sifa mbaya Kwa makosa ya wachache? ( kama kweli yanayosemwa ni sahihi) ingawa kama Mtanzania naamini wanatusingizia.
Je siku moja Soka la Taifa hili haliwezi kuwa looser na hasa CAF wakija kuthibitisha hizi tuhuma za uongo? Nna hofu tusije kuingia Msambweni tukaja kulia na Mabua bila sababu, ( Mungu atuepushia mbali)
Ila mimi naamini Clubs zote za Afrika hususan zilizokuja hapa,zinaona gere kwa club Ya Tanzania kushinda nyumbani,,tusikubali kushutumiwa kibwege bwege, Waafrika tumejawa na hasadi nyingi za kimaendeleo.
Ila nna rai moja tu,, tujitahidi sana kupunguza kulalamikiwa lalamikiwa kila wakati, inaweza kuhalalisha uongo wao bila sababu, coz walalamikaji wameshakuwa wengi mno, inafika wakati Kocha wa team pinzani mbele ya Kocha wa Club ya Tanzania, anapata Guts za kusema hayo huku camera zikiwa macho, tena anasema Kwa uwazi bila hofu, something wrong? Or ni roho mbaya juu yetu?
All in All Hongereni Watani zetu kwa ushindi wa jana no matter wat, iwe kwa Penati ya michongo au Bad hospitality nje ya Uwanja, lakini mmeshinda.
Iddi Amin Dada ( Nduli) aliwahi kusema, “kula Nyama ya Mtu kunanoga bila kujali anaeliwa nae ni Mtu”.
Tuwe na Jumatatu njema ya Pasaka ???