Universal Music Group pamoja na Kanye West wanakabiliwa na kesi ya wimbo wa “Power” alioutoa mwaka 2010.
Kwenye wimbo huo, Kanye alitumia vionjo kutoka kwenye wimbo wa King Crimson “21st Century Schizoid Man,” wa mwaka 1969, kwa mujibu wa Variety, inaelezwa kuwa Declan Colgan Music Ltd, ambao wanamiliki toleo la awali la wimbo huo, waliwasilisha kesi katika mahakama kuu ya Uingereza mapema mwezi Machi 2022.
Madai hayo yanakuja kufuatia Kanye kuweka wimbo huo kwenye mtandao wa Youtube mwaka 2010 kabla ya kuwepo kwa makubaliano ya awali ya matumizi ya sampuli hiyo, ambapo wimbo huo mpaka sasa umepata jumla ya watazamaji takriban milioni 134.
Kesi hiyo inasema, wimbo huo baadaye ulionekana kwenye album ya Kanye iitwayo ‘My Beautiful Dark Twisted Fantasy’ aliyoiachia Novemba 22, 2010.
Inaelezwa wakati huo DCM ilimuomba Ye, na kampuni yake ya uzalishaji, Rock the World kutia saini mkataba ambao ulisema sampuli hiyo itapata mrahaba wa 5.33% katika kila sehemu ambayo nakala ya wimbo wa huo itauzwa au kutumiwa kwa namna yeyote.
DCM sasa inadai kwamba UMG imeshindwa, na inaendelea kushindwa, kutii wajibu wake wa kihasibu wa mrabaha kuhusiana na masharti sahihi waliyopaswa kuyafuata.
Kwa mujibu wa Complex, kwa Sasa, wanachotaka DCM ni mirahaba yao ya utiririshaji (Streaming Royalties) iwe sawa na mauzo halisi ya CD, badala ya asilimia zinazotolea na majukwaa ya malipo kama Spotify kwa kila stream moja.
DCM inataka kulipwa kwa mfumo huo ikiwa ni pamoja na riba ikiambatana na kubadilisha makubaliano ya leseni ili kuakisi hatua ya kusonga mbele.