Kamanda wa Jeshi la Polisi Dar es Salaam,Muliro Jumanne Muliro amesema Jeshi hilo linawashikilia watu sita kwa mahojiano kufuatia tukio la watu kujeruhiwa kwa mapanga na kikundi kinachodaiwa kuwa ni ‘Panya Road’ katika eneo la Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam ili watu hao waeleze walipo wenzao na wanapeleka wapi vitu hivyo baada ya kuiba.
Kamanda Murilo amesema hayo leo Mei 2, 2022, mara baada ya usiku wa kuamkia leo vijana hao kujeruhi kwa mapanga watu 19, katika mtaaa wa Mtongani, Kata ya Kunduchi.
“Baadhi ya vijana tuliowakamata waliacha shule darasa la tano, wengine wanavuta bangi wanaseman kabla ya kufanya matukio lazima wawe kwenye mazingira ambayo yanaweza kuwapa ujasiri wa kufanya matukio mabaya ndiyo maana mtu anaporwa simu kwa kukatwa panga,” amesema Kamanda Muliro