Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wafanyakazi kuwa ahadi ya kuwaongezea Mshahara aliyoitoa mwaka jana wakati wa sherehe za Mei Mosi jijini Mwanza ipo pale pale.

Amesema hayo wakati wa sherehe za mwaka huu za siku ya wafanyakazi Duniani zinazofanyika Mkoani Dodoma.

Rais Samia amesema kwamba mahesabu ya nyongeza ya kima cha mshahara yanafanyiwa ukokotoaji na wafanyakazi wataona matokeo kwenye mishahara yao.

Pamoja na ahadi hiyo ya mabadiliko ya mishahara kuongezeka Rais Samia amekataa kile kiwango cha chini cha milioni 1 na elfu 10 kilichotajwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA).

“Lakini pamoja na hayo lile jambo letu lipo ndugu zangu jambo letu lipo si kwa kiwanho kilichosemwa na TUCTA  kwasabu mnajua hali ya uchumi ya nchi yetu na hali ya uchumi wa dunia.” amesema Rais samia.

Ahmed Ally: Gape limekuwa kubwa sana
TUCTA yamkumbusha Rais Samia ahadi yake