Viungo wanne wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC leo Jumatano (Mei 11) wataukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar, utakaounguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa mishale ya saa moja usiku.
Mchezo huo ni wa Mzunguko wa Pili baada ya ule wa Mzunguko wa kwanza Kagera Sugar kuwatungua bao 1-0 Simba SC, Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Kocha Mkuu wa Simba SC Pablo Franco Martin amethibitisha kuwakosa wachezaji Mkude Jonas, Morrison Bernard, Kanoute Sadio na Lwanga Taddeo.
“Wachezjai hawa bado hawako FIT kufuatia majeraha yanayowakabili, hivyo tutawakosa katika mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar.”
“Lakini kuwakosa hawa haina maana kwamba hawatakuwepo wengine, wapo wachezaji ambao tumewaandaa kwa ajili ya mchezo wetu huo muhimu.”
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuweza kushuhdia mchezo wetu huu ambao utakuwa na ushindani mkubwa.” amesema Kocha Pablo
Simba SC inashuka Dimbani SC ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Barakwa kufikisha alama 46, huku Kagera Sugar iliyopoteza mchezo uliopita dhidi ya Geita Gold kwa kufungwa 1-0 ipo nafasi ya 7 kwa kufikisha alama 29.