Ripoti ya Kitengo cha ufuatiliaji wa masuala ya afya cha Ikulu (SHHMT), iliyokuwa ikuchunguza tuhuma za upotevu wa figo ya Bi. Peragiya Muragijemana katika Hospitali ya Mubende ya jijini Kampala nchini Uganda, imekataliwa na familia ya mgonjwa.   

Akiongea kwa niaba ya familia, Baba wa Bi. Peragiya Bwana Sebastian Rwimo amesema hawajaridhishwa na ripoti ya matibabu ya Ikulu ya Marekani inayowasafisha madaktari wa hospitali ya Mubende.

“Tumekuwa tukiomba matokeo tangu Juni 5, 2022 lakini tuliambiwa tuweke ombi letu kwa maandishi na inasikitisha sana kwamba SHHMT sasa inatoa ripoti kuhusu uchunguzi, ikiwa ni pamoja na matokeo bila kutupatia nakala yoyote,” alisema Rwimo.

Hata hivyo, maafisa kutoka SHHMT jana Juni 8, 2022 walitupilia mbali shutuma za Bi. Muragijemana dhidi ya madaktari wa Mubende wakidai uchunguzi wa CT ya tumbo uliofanywa na Dkt. Sharif Kikomeko wa hospitali ya Mulago, ulibaini kutokuwepo kwa tishu za figo kwenye kitanda alicholalia.

“Bi. Muragijemana alichunguzwa vizuri ili kuondoa incision yoyote kwenye fumbatio isipokuwa kovu la incision ya upasuaji kwenye fumbatio la chini na uchunguzi haukupata kovu jingine zaidi ya upasuaji wa chini wa tumbo unaojulikana kama bikini (pfannenstiel) incision,” alisema Dkt. Warren Namaara.

Aidha, Dkt. Namaara amesema timu yake ilikutana na Bi Muragijemana na baadhi ya watu wa familia yake na kujadili ripoti hiyo kutoka kwa Mulago, madai ambayo familia hiyo iliyapuuza na kusema ni ya uongo.  

Familia hiyo imesema, “Tunapanga kufanya uchunguzi mwingine wa CT scan kutoka hospitali ya kibinafsi kwa sababu hatuwezi kuamini matokeo kutoka Mulago kwa kuwa walikataa kutupa nakala na kuamua kukimbilia kwenye vyombo vya Habari”.

Hata hivyo bado haijafahamika ni vipi kamati ya SHHMT ilishughulikia kesi hiyo ya Mubende iliyokuwa ikishikiliwa na Polisi jijini Kmpala ambao ndiyo walitakiwa kuchunguza na kutoa majibu kwa wahusika ambao wanatuhumu uwepo wa viashiria vya upindishaji wa haki.                 

Bi. Peragiya Muragijemana (20), mkazi wa Kijiji cha Lwemiggo Parokia ya Kabyuuma kaunti ndogo ya Kalonga katika Wilaya ya Mubende, anadai kuwa figo yake ya kulia iliondolewa wakati akifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Mubende Aprili 24, 2022.

NBC: Bado tupo sana katika Soka la Bongo
Aituhumu serikali kumcheleweshea kifo