Ofisa Mtendaji mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa amesema klabu imepokea ofa mbili kwa nyota wao, Fiston Mayele.
Amesema Kaizer Chief na Berkane zimeonyesha kumtaka nyota huyo wa kupachika mabao Yanga.
“Lakini kama klabu hatumuuzi,” amesema Senzo.
Katika hatua nyingine, Senzo ni kama amewakosha mashabiki wa Yanga baada ya kusisitiza kuwa kombe la ubingwa watalichukua palepale baada ya mechi yao kabla ya Ligi kuisha.
Yanga inahitaji ushindi kwenye mechi ijayo na Coastal ili kutangaza ubingwa.
Kama itashinda, Bodi ya Ligi imesema watakabidhiwa kombe lao siku hiyo hiyo kama watashinda.
Huku akikoleza kauli ya Bodi, Senzo alisisitiza ubingwa ni pale pale, akimaanisha kwenye mechi ijayo, jambo ambalo lilisababisha watu kuangua kicheko.
Chanzo: Mwanaspoti