Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni ameitaka Idara ya Uhamiaji nchini kusimamia uingiaji na utokaji wa wageni katika mipaka ya nchi kwa kufuata sheria.

Masauni ameyasema hayo akiwa Loliondo, Ngorongoro Mkoani Arusha wakati akikagua maendeleo ya zoezi la uwekaji wa alama za mipaka katika eneo la pori tengefu la eneo hilo.

Amesema Serikali itafanya uhakiki wa kina ili kubaini uendeshaji wa asasi za kiraia nchini, ikiwemo namna wanavyofanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na kwamba zitakazokiuka zitachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri Masauni ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya zoezi na kuwataka wahusika kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mwl. Raymond Mangwala akiongea katika eneo hilo amesema wamepokea maelekezo yake na kwamba watahakikisha hali ya usalama wa wananchi na mali zao inaendelea kuimarishwa.

Mwl. Mangwala ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela alimueleza Waziri Masauni kuwa na kuwa zoezi hilo litaendelea kwa hali ya amani na utulivu katika eneo hilo la Wilaya ya Ngorongoro.

Bajeti Zanzibar yatupia macho maeneo muhimu

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akiwana baadhi ya Viongozi na Askari Wilayani Ngorongoro, alipotembelea eneo hilo kuangalia maendeleo ya zoezi la uwekaji alama kwenye mipaka ya pori tengefu la Loliondo lililopo Mkoani Arusha.

UN yahofia ghasia Loliondo, Temu awatoa hofu
Diamond ampongeza Manara, Young Africans