Waziri wa Ulinzi, Dkt. Stergomena Tax, ameliomba Bunge kuondoa maneno ya Mbunge Alexander Mnyeti kwenye kumbukumbu rasmi za majadiliano na hoja kati ya wabunge na serikali ‘Hansard’.
Dkt. Stergomena amesema maneno hayo ni hatari na yanaingilia mahusiano ya kidplomasia kati ya Tanzania na Nchi jirani ambazo Nchi imekua na mahusiano nayo mazuri.
Taarifa ya Waziri Stergomena inakuja baada ya Mbunge huyo kusema watu wanaacha nchi zao wanakuja hapa nchini kwa jailli ya ajira na kuanza kutetema wakati Nchi zoo zinaibiwa madini.
Mnyeti aliyasema hayo jana Bungeni wakati mijadala ya hoja ya kuchangia bajeti ya Wizara ya Fedha ikiendelea katika kikao cha jioni Jijini Dodoma.
Kabla ya kuwa Mbunge, Alexander Mnyeti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha ambaye aliteuliwa na Hayati Dtk. Magufuli wakatyi wa awamu yake ya kwanza aya Urais na badale katika Awamu ya Pili Mnyeti alimshinda Dkt. Charles Kitwanga akawa mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoa wa Mwanza.