Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Mkurugenzi Mtendaji wa BioNtech, Ugur Sahin wamezindua mradi wa ujenzi wa kiwanda cha chanjo cha RNA mjini Kigali.

Mradi huo, unatajwa kuwa ni wa kwanza barani Afrika kati ya miradi mitatu iliyopangwa katika bara hili, unaolenga kutoa matibabu dhidi ya maradhi ya Uviko-19 na magonjwa mengine ifikapo mapema mwaka 2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa BioNTech, Ugur Sahin, amesema mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Bill na Melinda Gates Foundation, kutengeneza chanjo ya kifua kikuu, VVU na chanjo ya malaria.

“BioNTech inafanya utafiti na kutengeneza chanjo na dawa za kuzuia malaria, kifua kikuu na VVU, na magonjwa haya ni sababu kuu za vifo vingi vinavyotokea katika bara la Afrika,” amesema Sahin.

Kwa upande wake, Rais Paul Kagama ameuita mradi huo kuwa ni “grounbreaking” na kusema nchi yake ilifanya kazi ya kuvutia watafiti wa dawa za kibiolojia katika sekta ya viwanda.

Uzalishaji huo, utajumuisha chanjo dhidi ya Uviko-19, sambamba na dawa zitakazotibu maradhi ya malaria, kifua kikuu, VVU na magonjwa yaliyo mengi barani Afrika.

Majaribio ya binadamu ya chanjo ya malaria ya BioNTech kwa kutumia teknolojia ya mRNA, yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa 2022, katika bara hili lililo na chanjo chache zaidi duniani dhidi ya Uviko-19, kwa kuwa chini ya asilimia 20 ya wakazi wake bilioni 1.2 waliopokea dozi mbili za chanjo.

Dkt.Stergomena:Maneno ya Mnyeti yafutwe kwenye 'Hansard'
Serengeti Girls kundi moja na Ufaransa