Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amewaambia Mawaziri wa Mambo ya Nje wa viongozi wa mataifa 20 yaliyoendelea kiuchumi duniani G20, kuwa shirikiano wenye nguvu kati ya Mataifa ni njia pekee endelevu kuelekea ulimwengu wenye amani, utulivu na ustawi kwa wote.

Guterres, ameyasema hayo katika mkutano na Viongozi hao uliofanyika Bali nchini Indonesia, na kusema wakati uliopo ni mgumu kwa mfumo na utawala wa kimataifa, ikiwemo mpangilio wa kimataifa wenye hatari ya kutengana kutokana na changamoto mbalimbali kama mabadiliko ya tabianchi, janga la COVID-19, vita nchini Ukraine, na aina mpya za migogoro.

“Kuimarisha mfumo wa ushirikiano wa mataifa si mada pekee ya kikao hiki, bali ni njia pekee ya kuepuka uhaba wa chakula ulioenea, kuongezeka kwa machafuko ya hali ya hewa, na wimbi la umaskini ambao hautaacha nchi yoyote bila kuguswa,” amebainisha Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, ametaja maeneo matatu ya hatua za dharura za kimataifa: dharura ya tabianchi ambayo ni chakula, nishati na fedha, na kusema ahueni za misaada isiyo sawa kutokana na majang. mbalimbali hayawezi leta suluhisho.

Aidha, amesema janga la tabianchi ni dharura kuu, huku akionya kwamba vita ya uwepo wa joto la kimataifa la nyuzi joto 1.5 litashinda au kushindwa kufikia mwishoni mwa muongo.

“Mnawakilisha uchumi mkuu na asilimia 80 ya uzalishaji wa hewa chafuzi duniani, ninyi Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi tajiri jukumu la kuzuia athari mbaya zaidi za janga la tabianchi linategemea sana mabega yenu,” amesisitiza Guterres.

Bendera za Mataifa mbalimbali wanachama wa Umoja wa Mataifa zikipepea nje ya Makao Makuu ya Umoja huo jijini New York nchini Marekani

Ingawa, mpango wa kimataifa unahitaji kupungua kwa asilimia 45 chini ya viwango vya mwaka 2010 ili kufikia lengo la nyuzi joto 1.5, ahadi za sasa za tabianchi za kitaifa zinaweza kusababisha ongezeko la asilimia 14 ifikapo mwaka 2030.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, ametoa wito wa mapinduzi ya nishati mbadala na kukomesha uraibu wa kimataifa wa nishati ya mafuta kama kipaumbele cha juu.

Hata hivyo hakuna viwanda vipya vya makaa ya mawe, au upanuzi wa utafutaji wa mafuta na gesi, huku nchi zinazoibukia kiuchumi zikilazimikz kuwa na uwezo wa kufikia rasilimali na teknolojia ili ziweze kubadilishwa na kuwa mbadala.

Mabadiliko Tabianchi

Nchi tajiri pia zitalazimika kufanikisha ahadi ya dola bilioni 100 ya ufadhili wa tabianchi kwa nchi zinazoendelea kuanzia mwaka huu na zitahitaji msukumo wa kukabiliana na hali na mifumo ya tahadhari ya mapema.

Mtoto auawa kwa risasi mbugani akipambana na askari
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Julai 10, 2022