Takriban watu 18 wamefariki, baada ya gari la abiria walilokuwa wakisafiria kugongana na trela kati ya Taru na eneo la Samburu kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa kaunti ya Kwale, nchini Kenya.

Mkuu wa Polisi wa Kinango Sation, Fred Ombaka amesema miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo ya saa kumi na mbili jioni walikuwa watoto wawili na kwamba gari hiyo maarufu Kama matatu, iligonga trela wakati dereva wake akijaribu kulipita.

“Tumegundua kuwa matatu ilikuwa ikijaribu kuvuka lakini kwa bahati mbaya dereva alishindwa kuidhibiti ilipokaribia trela, na kusababisha kugongana ana kwa ana na ilikuwa ikiendeshwa kwa mwendo wa kasi na ilipokuwa ikipita, iligonga trela kwenye njia nyingine,” amesema Ombaka.

Mabaki ya gari ya abiria iliyohusika kwenye ajali katika barabara kuu ya Nairobi – Mombasa

Amesema, Gari hilo la Huduma za Umma lililosajiliwa kwa Kampuni ya Wumeri Shuttle na nambari ya usajili KCY 297N  lilikuwa likitoka jijini Nairobi na kuwachukua abiria wengine katika Mji wa Voi likielekea Mombasa.

Kufuatia ajali hiyo, Mkuu huyo wa Polisi aliwashauri madereva kuwa waangalifu wanapoendesha kwenye barabara kuu huku akitahadharisha iwaki wamechoka wanapaswa kupumzika.

“Kama umechoka unaweza kusimama na kupumzika kwa muda kabla ya kuendelea na safari, mana uamuzi wako usio na busara unaweza sababisha maafa kama haya ni vyema kuwa waangalifu sana, ” amesisitiza Ombaka.

Ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha gari la abiria na lori eneo la Taru kando ya Barabara kuu ya Nairobi-Mombasa

Miili hiyo 18 ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya kaunti ndogo ya Kinago kaunti ya Kwale huku Kamanda wa trafiki kanda ya Pwani Peter Maina akisema uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea.

Watu 14 wauawa, wauaji wafyatua risasi hovyo katikati ya Mji  
Ruto ajibu tuhuma za kumpiga kofi Rais Kenyatta