Mashahidi waanza kutoa ushahidi wa tukio la Msemaji wa Young Africans Haji Manara dhidi ya Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.

Ilitokea sintofahamu Julai 2 wakati wa fainali ya kombe la FA iliyoikutanisha Young Africans na Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha ilionekana wawili hao wakizozana katika video iliyosambaa mitandaoni huku watu wakimtuliza Manara.

Julai 3 Sekretarieti ya TFF ilifungua shauri mbele ya kamati ya maadili dhidi ya Manara kutokana na vitendo vya ukiukaji wa maadili.

Tayari kesi huyo imeishaanza kuunguruma na mashahidi wameanza kutoa ushahidi mbele ya kamati hiyo.

Mmoja wa mashahidi alipotafutwa alikaririwa juu ya kushangazwa na namna mzozo huo jinsi ulivyoibuka.

Licha ya Manara kukutana na Karia na kuomba msamaha na kuomba hadharani akikiri kukosea kamati imeendelea na kesi hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti

Zoran asisitiza usajili wa Mohammed Ouattara Simba SC
Young Africans yashusha Beki Tatu kutoka DR Congo