Imefahamika kuwa Beki kutoka Ivory Coast Mohammed Ouattara amependekezwa na Kocha Mkuu wa Simba SC Zoran Maki, ili aongezwe kwenye usajili wa klabu hiyo.

Zoran Maki anaamini uwezo wa beki huyo, kutokana na kutambua uwezo wake, baada ya kufanya kazi pamoja wakiwa Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Kwa sasa Beki huyo anaitumikia Klabu ya Al Hilal ya Sudan ambayo pia iliwahi kuongozwa na Kocha Zoran Maki.

Taarifa zinaeleza kuwa, Beki huyo tayari amekubali kutua Msimbazi, ili kuchukua nafasi ya Pascal Serge Wawa, aliyeeondoka klabuni hapo kufuatia Mkataba wake kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita 2021/22.

Zoran anaamini endapo usajili wa Mohammed Ouattara utakamilishwa kwa asilimia 100 ndani ya Simba SC, kikosi chake kitakua salama kwenye michuano ya msimu ujao, ambao rasmi umepangwa kuanza mwezi Agosti.

Wakati huo huo Kocha Zoran ameutaka Uongozi wa Simba SC, kuhakikisha unakamilisha usajili wa nyota wengine aliowapendekeza, sio kinyume na hivyo.

Wydad Casablanca kumlipa Mabilioni Simon Msuva
Kesi ya Manara Vs Rais wa TFF yaanza kuunguruma