Kampuni ya SportPesa imeitakia kila la kheri klabu ya Simba SC, baada ya kumaliza mkataba uliodumu kwa miaka mitano baina ya pande hizo mbili.
Simba SC jana Alhamis (Julai 14) ilitangaza kuingilia Mkataba wa Kampuni ya M-Bet kwa miaka mitano ambao rasmi umeshaanza, kufuatia kikosi cha klabu hiyo kuvaa Jezi zenye nembo ya Mdhamini huyo.
Mkurugenzi wa Sportpesa Tanzania Abbas Tarimba amezungumnza na Vyombo vya Habari jijini Dar es salaam na kuthibitisha kumaliza mkataba kati yao ya Simba SC.
Tarimba amesema pande zote zimeridhika kwa huduma iliyotolewa kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka mitatu, na wanaamini Simba SC itaendelea kuwa mfano wa kuigwa katika udhamini uliokuwepo kati yao.
Amesema anajivunia mafanikio makubwa waliyoyapata wakiwa na Klabu ya Simba SC, na hata upande wa Klabu hiyo ana uhakika utakuwa umefurahia kufanya kazi na kampuni hiyo ya Michezo ya kubashiri.
“Ni kweli tumemaliza Mkataba wa Simba SC, tumekuwa nao kwa kipindi Kirefu, sisi tulikua na matarajio ambayo tulipenda yafanyike na wao ilikua hivyo pia,”
“Naweza kusema kwamba tuheshimu maamuzi yaliyofikiwa na pande zote mbili, tunaitakia kila la kheri Simba SC katika mpango wake ndani na nje ya uwanja.” amesema Tarimba