Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Kijiji cha mwisho kupata umeme nchini itakua ni mwezi March mwaka 2023, kauli ambayo imefanya Wananchi wengi wenye ukosefu wa Nishati hiyo kuwa na matumaini ya ku9ondokana na giza la muda mrefu.

Sambamba na kauli hiyo pia Waziri Makamba amewahakikishia Wananchi wa Kijiji cha Bulela kiliochopo Geita kuwa kabla ya siku kuu ya Krismasi Desemba 25, 2022 watakuwa wamepata huduma ya umeme ambao wataunganishiwa kwa Shilingi 27,000 pekee.

Waziri Makamba, ameyasema hayo Julai 14, 2022 akiwa katika ziara ya kikazi aliyoifanya Kijijini hapo na maeneo mengine ya kanda ya ziwa, kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto za umeme kwa Wananchi.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba akiongea jambo katika moja ya ziara zake Kanda ya ziwa.

“Niwahakikishie kwamba Krismasi ya mwaka huu (Julai 25, 2022), mtasherehekea mkiwa na umeme ambao mtaunganishiwa kwa shilingi elfu 27 tu,” amesema Makamba.

Akiwa katika Kijiji hicho, Waziri Makamba pia amemtaka Mkandarasi kufika saiti kwenye Kijiji cha Bulela awe amefikisha umeme katika eneo hilo kabla hajamaliza ziara yake.

Mkandarasi huyo, pia ametakiwa kufika kwenye Ofisi za Serikali ya Kijiji cha Bulela kesho asubuhi Julai 16, 2022 ili kuonana na Viongozi wa Serikali ya Kijiji kwa ajili ya Usanifu wa awali, ununuzi wa vifaa na kuhakikisha uunganishaji wa umeme unafanyika.

Watatu washikiliwa vifo vya vijana 21 kwenye baa

Waziri wa Nishati, January Makamba akizungumza na Kikundi cha Mamalishe Busisi ikiwa ni sehemu ya umasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo pia aliwapatia mitungi ya gesi ili kurahisisha shughuli zao za upishi nili kuepukana na athari za matumizi ya kuni na mkaa.

Amesema, Tanzania ina takribani Vijiji 12,600 na kwamba kati ya Vijiji hivyo hakuna hata kimoja ambacho hakitafikiwa na umeme na kwamba vijiji vyote visivyo na nishati hiyo vipo katika mpango wa kufikiwa na huduma hiyo muhimu.

“Labda niseme kitu kimoja, tuna takribani Vijiji 12,600 hivi na kati ya Vijiji hivyo hakuna hata kimoja ambacho hakitafikiwa na umeme na hata vile visivyo na umeme vyote vipo katika mpango wa kufikiwa maana fedha zipo,” amefafanua Waziri Makamba.

Akiwa wilayani Sengerema, Waziri Makamba aligawa mitungi ya gesi takriban 80,  ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kudai hiyo ni programu maalumu ya majaribio.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba akizungumza na Wananchi.

Amesema, program hiyo ya miezi sita itawezesha upatikanaji wa taarifa za kutengeneza mpango mkubwa wa kitaifa wa usambazaji wa gesi nchini itakayowanufaisha akinamama.

Kagera Sugar yatuliza PRESHA ya mashabiki
SportsPesa yathibitisha kuachana na Simba SC