Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anashiriki Kongamano la Pili la kumienzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa leo hii leo Julai 14, 2022 katika ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar.

Hayati Benjamin William Mkapa, alizaliwa katika familia ya Mzee William Matwani na Mama Stephania Nambaga Novemba 12, 1938, katika kijiji cha Lupaso, Masasi, mkoani Mtwara na alikuwa alikuwa mzaliwa wa mwisho katika familia ya watoto wanne.

Alianza kazi kama Afisa Tawala Serikalini Wilaya ya Dodoma, Mkoani Dodoma mwezi Aprili, 1962 na kisha baadaye baada ya miezi minne Agosti, 1962 alijiunga na masomo ya Shahada ya Uzamili ya Diplomasia katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Mwaka 1963 alifanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje katika Dawati la Afrika akiwa na cheo cha Afisa wa Mambo ya Nje akifanya kazi ya kuchukua muhtasari wa mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje au Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapokuwa na wageni.

Katika kupambana na ufisadi nchini, Hayati Benjamin William Mkapa aliunda TUME ya Rais ya kuchunguza rushwa iliyokuwa chini ya Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba mwaka 1996, ambapo matokeo yake yalisaidia kuimarisha vita dhidi ya rushwa nchini kwa kuanzisha Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU.

Aidha, alichochea marekebisho ya uchumi ikiwemo kuongeza nafasi ya sekta binafsi na ubinafsishaji hasa kwa Mashirika ya Umma, ambayo yalikuwa hayajiendeshi vizuri na yaliyokuwa yamekufa, ikiwemo kuanzisha utaratibu aliousimamia mwenyewe wa majadiliano kati ya Serikali na sekta binafsi kupitia Baraza la Biashara la Taifa (NBC).

Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Benjamin William Mkapa aliimarisha Uhuru wa Vyombo vya Habari na wa kisiasa, na pia alitambua na kulenga kuunga mkono mchango wa taasisi za dini katika maendeleo ya Taifa, na kukabidhi baadhi ya majengo ya Serikali kwa taasisi hizo ili zianzishe vyuo vikuu kwa mfano ikiwemo Shule ya Sekondari Mazengo kwa Kanisa la Anglikana kuwa Chuo Kikuu cha St. Johns.

Baada ya kustaafu mwaka 2005, Hayati Benjamin William Mkapa alijishughulisha na mambo mbalimbali ikiwemo kuunda Taasisi yake inayohusika na kupambana na ugonjwa wa UKIMWI na kuboresha utoaji wa huduma za afya hasa katika maeneo ya pembezoni mwa nchi, The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF).

Kongamano hilo pia limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa, Taasisi za Tanzania bara na Visiwani, akiwemo Rais wa pili wa Msumbiji Joaquim Chisano, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye na wageni waalikwa.

Hayati John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Benjamin William Mkapa, alikuwa ni rais wa tatu wa Tanzania, akikaa madarakani kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 na aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 81, huku kifo chake kikiacha pigo si kwa Tanzania pekee bali na bara la Afrika kwa ujumla.

Geita Gold yampigania George Mpole
George Mpole: Sijui nitacheza wapi msimu ujao