Akaunti ya Twitter, iliyokuwa na jina la IEBC Tabulation, ambayo imekuwa ikichapisha baadhi ya matokeo ya uchaguzi wa Kenya, kwa kutumia nembo ya Tume ya uchaguzi ya Kenya (IEBC), imefungiwa rasmi.
Akaunti hiyo, ilikuwa ikiorodhesha matokeo hayo kitu ambacho baadhi ya Wananchi wa Kenya walikuwa wakiamini ni tovuti ya IEBC na inadaiwa imepotosha umma kutokana na maelezo yake katika machapisho yake.
Baadhi ya raia wa nchi hiyo, wamesema walianza kuitilia mashaka baada ya machapisho yake kadhaa ambayo yalikuwa yakionekana kuwa na walakini na wengine kutilia wasiwasi, juu ya uhalali wa akaunti hiyo.
Baadhi ya machapisho ya hivi karibuni, yalikuwa yanaonyesha upendeleo wa wazi kwa baadhi ya wagombeaji jambo ambalo lilitiliwa mashaka na wengi, na sasa imesitishwa rasmi.
Kumekuwa na hali ya upotoshaji, katika utoaji wa matokeo kwa baadhi ya vyombo vya Habari, hasa katika mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakiyanakili na kisha kuyasambaza.