Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), Wafula Chebukati amesema hawatamtaja mshindi wa uchaguzi wa Urais Kenya hii leo licha ya matokeo kuanza kujumlishwa na mawakala vikiwemo vyombo vya Habari vinavyotumia Fomu za 34A zilizopo.

“Matokeo katika tovuti ya umma ni yale yale ambayo tume itatumia kutangaza matokeo pekee, tumewapa mawakala, vyombo vya habari na baadhi ya wadau kupata usawa ila tamko la matokeo ya Urais halitafanyika leo,” amesema Chebukati.

Katika kikao cheke na Hanahabari hivi karibuni kabla ya kupiga kura hapo jana, Mwenyekiti huyo wa IEBC pia alikaririwa akisema matokeo yatakayotangazwa katika vituo vya kupigia kura yatakuwa ya mwisho.

Aidha, Chebukati alibainisha kuwa IEBC bado haijapokea nakala halisi za Fomu 34A au 34B na kuongeza kwamba, “ukusanyaji wa matokeo kutoka maeneo bunge 290 unaendelea na wasimamizi wa uchaguzi watatoa fomu 34B baadaye.”

Hata hivyo, mwenyekiti huyo amezidi kusisitiza kuwa, “Tunawahimiza wagombea ambao wameshindwa katika uchaguzi wakubali matokeo.”

Huku tume ikiwa bado kujumlisha takwimu za urais, matokeo ya muda ya Taifa kulingana na fomu 34A zilizopakiwa kwenye tovuti ya IEBC yanaonyesha kuwa Naibu Rais William Ruto anaongoza kwa asilimia 51.45 na Raila Odinga kwa asilimia 47.9.

Simba SC kushiriki CAF SUPER LEAGUE
Young Africans kupelekwa Arusha Ligi Kuu?