Gavana wa Kitui Charity Ngilu, ameilaumu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), baada ya jina lake kuchapishwa kwenye karatasi za kura licha ya kujiondoa kwenye kinyanganyiro cha Ugavana

Gavana huyo amesema mkanganyiko huo utasababisha kura nyingi kupotea na wafuasi wake kuchanganyikiwa hata hivyo Ngilu amewahimiza wafuasi wake na kuliipuuza jina lake na badala yake kumpigia kura David Musila wa chama cha Jubilee.

Ngilu amesema mnamo Julai 29, alikuwa ameiarifu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kulifuta jina lake kwenye karatasi za kupigia kura.

“Nilitarajia IEBC kufanya hima baada ya kuwajulisha kwa kuiandikia barau. Makosa kama hayo hayapaswi kufanyika kwa sababu kura nyingi zitaharibika,” amesema Ngilu

Ngilu alikuwa amewahimiza wafuasi wake kulipuuza jina lake wakati wa kupiga kura, na badala yake kumpigia kura David Musila, wa chama cha Jubilee.

“Watu wa Kitui wanajua ninamuunga mkono mwaniaji wa Jubilee David Musila, na nimekuwa nikimpigia debe, na hilo halijabadilika,” amesema Ngilu

Motsepe: Afrika inapaswa kupiga hatua kwa kazi kubwa
Mali yapokea vifaa vya Kijeshi toka Urusi