Wachezaji 27 wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans yamewaslishwa Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’ kwa ajili ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2022/23.

Simba SC na Young Africans zitaiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa, huku Azam FC na Geita Gold FC zikishiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Majina ya Wachezaji wote watano wa Kigeni waliosajiliwa Klabuni hapo Stephen Aziz Ki, Bernard Morrison, Lazarius Kambole, Joyce Lomalisa na Gael Bigirimana yapo kwenye orodha hiyo.

Young Africans itaanza kupambana Kimataifa kwa kuwakabili Mabingwa wa Soka Sudan Kusini Zalan FC itakayokua nyumbani katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza kati ya Septemba 9 -11.

Mchezo wa Mkondo wa Pili umepangwa kuchezwa kati ya Septemba 16-18, ambapo Young Africans itakua nyumbani jijini Dar es salaam, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mshindi wa Mchezo huo atacheza na Mshindi wa Mchezo wa Al Hilal ya Sudan dhidi ya St George ya Ethiopia ili kumpata mshiriki ambaye atatinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Orodha ya majina wa Young Africans iliyowasilishwa ‘CAF’ Walinda Lango ni Djigui Diara, Abutwalib Msheri pamoja na Erick Johora.

Mabeki: Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Joyce Lomalisa, David Bryson, Djuma Shaban, Abdalla Shaib, Yanick Bangala pamoja na Shomari Kibwana.

Viongo: Abubalar Salum, Zawadi Mauya, Crispin Ngushi, Dickson Ambundo, Gael Bigirimana, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Feisal Salum, Yusuph Athuman, Bernard Morrison, Denis Nkane, na Farid Mussa.

Washambuliaji: Lazarius Kambone, Fiston Mayele, Stephan Aziz Ki, na Heritier Makambo.

Ahmed Ally: Kuna watu wamedhamiria kuichafua Simba SC
Clatous Chama atinga Shirikisho la Soka Afrika