Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limewataka Wadau wa soka kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 17, zimeongia dosari kufuatia nchi mwenyeji (India), kuingia kwenye matatizo na Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’.

Shirikisho la Soka nchini India ‘AIFF’ limesimamishwa kwa muda na ‘FIFA’ kufuatia Serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya Uongozi.

FIFA imechukua maamuzi hayo baada ya Mahakama ya juu ya India kulivunja Shirikisho la Soka ‘AIFF’ mwezi Mei mwaka huu na kuteua wajumbe watatu kusimamia mchezo huo, ikiwa ni kinyume na kanuni za Soka Duniani.

Mkuuwa Idara ya Habari na Mawasilino wa TFF Clifford Ndimbo amesema taarifa bado hawajazipata taarifa rasmi za Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya miaka 17, kuingia dosari za kutofanyika nchini India.

Amesema kwa sasa ni mapema mno kwa TFF kutoa taarifa hizo, hivyo Mashabiki wa Soka nchini wanapaswa kuendelea kuwa watulivu na kuamini taarifa rasmi kutoka FIFA zitatumwa nchini na kuwasilishwa hadharani.

“Hatuwezi kuzungumza jambo lolote ambalo hatujalipata kiofisi, timu ipo kambini na inaendelea na maandalizi” amesema Ndimbo

Kikosi cha Serengeti Girls kimeweka kambi Kisiwani Unguja (Zanzibar) kujiandaa na Fainali hizo zilizopangwa kuanza Jumanne (Oktoba 11) hadi Jumapili (Oktoba 30).

Serengeti Girls imepangwa Kundi D pamoja na Bingwa mtetezi Ufaransa, Canada na Japan.

Clatous Chama atinga Shirikisho la Soka Afrika
Inonga, Outtara kupigwa chini Simba SC