Imefahamika kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Australia, Scott Morrison aliteuliwa kwa siri mwaka 2020 na 2021 na Gavana Mkuu David Hurley kuwa Waziri katika Wizara za Afya, Fedha, Hazina, Rasilimali na Mambo ya Ndani.
Uteuzi huo haukufahamika na Baraza la mawaziri, Bunge na Wananchi wa Taifa hilo, na sasa imeonekana kuwa Morrison alitumia mamlaka yake ya siri kwa mawaziri katika kufanya maamuzi katika maeneo mengine ya rasilimali.
Hali hiyo, imezua maswali na mijadala mbalimbali, huku wanasiasa na viongozi wengi wakiwemo wakongwe Waziri Mkuu Anthony Albanese, Waziri Mkuu wa zamani Malcolm Turnbull na Waziri Mkuu wa zamani Tony Abbott wakisema wangeidhihaki hatua hiyo kama kusingekuwepo na hali ya kidemokrasia.
Wamesema, hatua hiyo ni jambo lisilovumilika kwa kuwepo kwa mawaziri wa siri huku wakidai Bunge ni lazima lichukue hatua kuzuia kutokea kwa hali kama hiyo kuweza kutokea tena kwani ni fedheha kwa Taifa na ulimwengu kiujumla.
“Katiba inampa ya Australia, inampa Gavana Mkuu mamlaka ya kuteua mawaziri na endapo utakosa umakini katika kuisoma Katiba hiyo unaweza usiambulie lolote na kudhani kwamba Gavana ana mamlaka kisheria katika kuteua mawaziri,” wamesema Viongozi hao akiwemo Mchambuzi Brooke Hughe.
Ameongeza kuwa, “Kiutendaji, mamlaka hayo yanawekewa mipaka na mikataba ya kikatiba isiyoandikwa. Moja ya makongamano muhimu zaidi ni kwamba mtu anayeamuru imani ya Baraza la Wawakilishi ateuliwe kuwa waziri mkuu na huyu huwa ni kiongozi wa chama au vyama vilivyo katika muungano ambavyo vina viti vingi.”
Aidha, Hughe ameongeza kuwa uwezo wa gavana mkuu wa kuteua mawaziri pia umewekewa mipaka na sheria ambayo ni ile ya Mawaziri wa Nchi ya mwaka 1952 inayoweka ukomo wa idadi ya watu wanaoweza kuteuliwa kuwa mawaziri.
“Watu wasiozidi 30 wanaweza kuteuliwa kuwa mawaziri na wasiozidi watu 12 wanaweza kuteuliwa kuwa makatibu wa bunge au mawaziri wasaidizi na Kwa upande wake, waziri mkuu anamshauri gavana mkuu kuhusu nani anafaa kuteuliwa katika wizara nyingine,” amefafanua Brooke.
Hata hivyo, msemaji wa gavana mkuu, alitoa taarifa siku ya Jumatatu Agosti 15, 2022 kuwa uteuzi wa mawaziri wengi katika wizara moja sio jambo la kawaida huku taarifa hiyo pia ikidai kuwa ni suala la serikali ya wakati huo ikiwa na jinsi ya kutangaza uteuzi wa mawaziri ni hoja ya kwanza iliyo na ukweli, lakini ya pili ni ngumu zaidi.