Mwanasiasa Mkongwe Raila Odinga, amefafanua namna ambavyo analikataa tangazo la Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, Wafula Chebukati kuwa Naibu Rais William Ruto ndiye rais mteule wa Kenya akisema muungano wake huwa unafuata chaguzi zote za kikatiba zilizopo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu mwenyekiti wa IEBC, atangaze matokeo hayo jana Agosti 15, 2022, mgombea huyo urais wa chama cha Azimio la Umoja One Kenya Coalition, amedai Chebukati alionyesha kutozingatia Katiba kwa kutangaza matokeo yaliyochakatwa upande mmoja.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ambaye alishiriki katika uchaguzi wa urais amehutubia taifa kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais, jijini Nairobi. Picha na Thomas Mukoya/REUTERS.

Aidha, Odinga pia amesema mwenyekiti huyo ndiye pekee aliyepata kura ya urais na kuwafahamisha makamishna bila kuruhusu mjadala wowote wa matokeo.

“Mwenyekiti alipuuza Katiba, Azimio tunakataa matokeo ya urais yaliyotangazwa na Bw Chebukati,” amesema.

Odinga pia amewataka wafuasi wake kudumisha amani na utulivu na muungano huo na kwamba anafuata njia za kikatiba kubatilisha matamshi ya IEBC chini ya Chebukati.

Shaba kuchenjuliwa Tunduru
Takwimu za sensa kusaidia utoaji wa huduma kwa Wananchi