Kiungo Guido Rodriguez amedai kuwa anafuraha katika Klabu ya Real Betis huku tetesi zikiongezeka kuhusu kutaka kuhamia kwa wababe wa La Liga, FC Barcelona.

Barca wamewasajili wachezaji huru kama vile Ilkay Gundogan na Inigo Martinez kutokana na msukosuko wa kifedha wa klabu hiyo na ripoti zinasema kuwa miamba hiyo wa Katalunya wanamuona Rodriguez, ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu, kama shabaha inayofaa katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Kuwasili kwake kunaweza kumfanya Oriol Romeu aondoke huku kiungo mwingine wa kikosi cha kwanza akitafutwa, wakati Rodriguez akikiri ameridhika na Betis, mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2022 aliongeza kuwa hana uhakika na siku zijazo.

Alisema: “Ninahisi niko nyumbani Betis. Ninajisikia vizuri sana hapa, nina furaha sana, nimekuwa hapa kwa miaka minne na nusu na ukweli ni kwanmba nina furaha, furaha sana.

“Lazima ufanye maamuzi maishani na vizuri, tutaona kitakachotokea mwishoni mwa msimu. Ukweli ni kwamba hadi leo, mimi wala klabu hatuna uhakika nini kinaweza kutokea.

“Hakuna chaguo moja ambalo uamuzi wangu unategemea. Inategemea mambo mengi. Tayari nimeshasema, ni mada inayojirudia na sitaki kuunda matarajio yoyote ya uwongo au kusema chochote kwa watu.”

Barca watatafuta kuunda kikosi kitakachoweza kuwapa changamoto Real Madrid kwa ajili ya ubingwa wa La Liga wakati wa majira ya joto baada ya kuthibitisha kuwa kocha Xavi hatajiuzulu wadhifa wake.

Gavi alipata jeraha la mguu Novemba mwaka jana na hajacheza tangu wakati huo, wakati kiungo mshirika Pedri amekuwa akiugua mara kwa mara kutokana na matatizo ya utimamu wa mwili.

Frenkie de Jong pia amekosa michezo hivi majuzi kutokana na jeraha, huku Gundogan akiwasili majira ya kiangazi akicheza zaidi La Liga kuliko mchezaji mwingine yeyote katika klabu hiyo.

Rais Samia: Mradi bonde la Mto Msimbazi kupunguza athari za mafuriko
Pacome Zouzoua avunja ukimya Young Africans