Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza mpango wa kufuta kiasi kikubwa cha deni la mkopo kwa wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu wanaodaiwa fedha na Serikali kiasi kinachokadiriwa kufikia Dola 1.6 Trilioni.
Hatua hiyo, imetajwa kuwa ni muhimu kuliko nyakati zotekwa Taifa hilo la Marekani, ambapo watu milioni 45 wanadaiwa kiasi hicho kikubwa cha pesa toka mikopo ya shirikisho iliyochukuliwa chuo kikuu ambapo mpango huo unaweza kupunguza sintofahamu iliyokuwepo hapo awali.
Kwa miezi kadhaa, Wanademokrasia wanaoendelea wamempa msukumo Biden kuhusu suala hilo, wakisema kwamba msamaha wa deni ni muhimu ili kushughulikia tofauti za rangi katika uchumi wakidai mpango huo ni mdogo kuliko walivyotarajia.
Hata hivyo, Biden alitaka kushughulikia maswala ya kiuchumi kwa kulenga saizi ya misaada, huku Ikulu ya White House ikipima maswali ya haki na wengine wakihoji kuwa msamaha huo hauleti haki na usawa kwa wale ambao tayari walianza kulipa deni hilo la chuo kikuu.
Ikulu ya Marekani imesema, hatua hiyo inaweza kufanya mfumuko wa bei kuwa mbaya zaidi kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula kwani Biden angeghairi deni la Dola 10,000 kwa wale wanaopata chini ya dola 125,000 kwa mwaka na dola 20,000 kwa wale ambao walikuwa wamepokea ruzuku ya Pell kwa familia za kipato cha chini.
Inaarifiwa kuwa, mpango huo utakabiliwa na changamoto za kisheria huku Biden akitumia hatua ya utendaji badala ya sheria, kusamehe mikopo na wanachama wa Republican wanashutumu mpango huo kwa kusema “unawapendelea matajiri.”