Taarifa kuhusu Utekelezaji wa Programu ya lipa kutokana na Matokeo (Education Performance for Result-EP4R), imepokelewa na kujadiliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za mitaa..
Mradi huo wa kuimarisha ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi – BOOST na Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (Secondary Education Quality Improvement Project-SEQUIP), umejadiliwa Agosti 30, 2022.
Miradi hiyo inatekelezwa chini ya Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kwa kushirikiana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inalenga kuinua ubora wa elimu na ujenzi wa miundombinu ya elimu katika Shule za Msingi na Sekondari.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, inaongozwa na Jaffari Chaurembo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Makamu Mwenyekiti Mhe. Denis L. Londo, Mbunge wa Jimbo la Mikumi na kuhudhuliwa na wajumbe wa kamati hiyo.
Wengine waliouhudhuria ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa, Naibu Waziri Mhe. David Silinde, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Msonde na Wakurugunzi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.