Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha St. John, Winfrida Michael (24) baada ya kuchomwa kisu na mpenzi wake Julias Gervas (26) ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho.

Kamanda Otieno amesema kuwa sababu ikitajwa ni wivu wa mapenzi na baada ya Julius kufanya mauaji hayo alijaribu kujiua kwa kujikata tumbo na sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Dodoma.

“Hilo tukio limejitokeza ni wivu wa kimapezi kijana kamchoma kisu mpenzi wake akafariki baadaye alitaka kujichoma kisu lakini akawa amejijeruhi tuu na kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma,”

Kitwanga awataka Polisi kuwa na nidhamu
Kenya: Rais Kenyatta 'ampotezea' mteule Ruto