Mchambuzi wa Soka la Bongo Edo Kumwembe ameweka wazi ufahamu wake kuhusu uwepo wa Kocha Msaidizi wa Simba SC Seleman Matola ambaye juma lililopita alipata changamoto ya kushinikizwa kujiuzulu, kufautia matokeo ya 2-2 dhidi ya KMC FC.

Edo Kumwebwe ambaye pia ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi ameweka wazi hilo kupitia Kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM leo Jumatatu (Septemba 12).

Kumwembe amesema anaamini uwepo wa Matola katika Benchi la Ufundi la Simba SC ni sababu ya kulinda Maslahi ya Uongozi wa klabu hiyo kwa lengo la kuwaendesha Makocha wageni ambao wamekua wakienda kinyume na maagizo.

Kumwembe amesema: “Ninachofahamu ni kwamba Matola yuko pale kwa ajili ya kulinda maslahi ya upande wa viongozi dhidi ya benchi la ufundi. Ni kosa la muda mrefu sasa limendelea kufanyika, lakini huo ndio ukweli na ndio utamaduni wa soka la Afrika”

“Nafahamu kwamba mabosi wa Simba wanamhitaji mtu ambaye atafikisha hisia zao kwa urahisi kwa benchi la ufundi. Hii ndio kazi ya kwanza ambayo inamuweka Matola katika benchi la Simba. Wakati mwingine inasaidia wakati mwingine haisadii”

“Kuna makocha ambao wana vichwa vigumu na mabosi wa Simba wanaona kuna umuhimu wa kuwawekea mtu kama Matola kwa ajili ya kumkotroo pale ambapo anazidisha kufanya mambo ambayo huenda hayana maslahi kwa klabu.”

Parimatch na fursa ya 'namba zina hela cheza Bingo'
Azam FC yawasili salama jijini Mbeya