Baada ya Serikali kuidhinisha kiasi cha Shilingi 59.58 bilioni za ruzuku ya mafuta kwa mwezi Oktoba 2022, sasa bei ya lita ya petroli itapungua kwa Shilingi 133 (Dar es Salaam), Shilingi 118 kwa mafuta yanayopakuliwa kupitia bandari ya Mtwara na Shilingi 204 (Tanga).

Bei elekezi ya bidhaa za petroli, zitakazotumika Tanzania Bara kuanzia hii leo Oktoba 5, 2022 ambazo zimetangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwa rejareja itakuwa Shilingi 2,886 kwa lita ya petroli, Shilingi 3,083 kwa lita ya dizeli na Shilingi 3,375 mafuta ya taa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, dizeli imepungua kwa Shilingi 275 Dar es Salaam, Shilingi 360 kwa Tanga na Shilingi 333 na kwa Mtwara lita ya mafuta ya petroli kwa itakuwa Sh 2,908 na dizeli itauzwa kwa Sh 3,099, huku mafuta yanayo pakuliwa Tanga, petroli Shilingi 2,924 mafuta ya dizeli Sh 3,108 na mafuta ya taa Shilingi 3,275.

EWURA imesema bei za mafuta katika soko la dunia zimepungua kwa kuzingatia kikikotoo kilichotumika mwezi Agosti, ambapo petroli imepungua kwa asilimia 7.4, dizeli asilimia 3.9 na mafuta ya taa asilimia 1.9 huku ikibainisha kuwa, athari za upungufu huo zimezidiwa na ongezeko la malipo ya Premium katika soko zilizopanda kwa kati ya asilimia 50 na asilimia 163 kulingana na bandari.

Pape Ousmane Sakho aiwahi Premeiro De Agosto
Ahmed Ally: Juma Mgunda atatuvusha