Utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi unaotarajia kuhusisha kaya 20 elfu Tanzania Bara na Zanzibar, ni muhimu kwani utawezesha Serikali na Wadau kupata hali halisi ya mwenendo wa maradhi hayo, na kusaidia kuweka mikakati ya kuendana na uhalisia katika mapambano dhidi ya tatizo hilo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman ameyasema hayo akiwa Wilaya na Mkoa wa Mjini Magharibi, katika uzinduzi wa Utafiti huo utakaofanyika nchini huku akisema kwa upande wa Zanzibar ni vyema uende na viashiria vya maambukizi kwa kuhusisha makundi maalum, yanayohisiwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.

Amesema, matarajio ni kuona utafiti huo wa 2022/2023 unahusisha watu 40 elfu na kwamba ni matumaini ya serikali kuwa kaya zilizochaguliwa na watu watakaohusika watatoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha zoezi hilo muhimu ambapo taarifa zitakazopatikana zitaendelea kuwa siri na zitatumika kitakwimu pekee.

Othman ameongeza kuwa, Tanzanzia itapambamba na tatizo hilo ili kusaidia nchi kupiga hatua kiuchumi na kuweka mikakati imara ili wananchi waepukane na maradhi mbalimbali ikiwemo janga la Ukimwi, huku akiishukuru Serikali ya Marekani kupitia kituo chake cha Kudhibiti na kuzuia Magonjwa kwa msaada wa kifedha.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar, Dkt. Ahmed Khatib amesema Zanzibar kumekuwa na mkikakati mbalimbali ambayo iliyosaidia kupambana na kudhibiti janga hilo tangu kubainika kwa mgonjwa wa kwanza 1986 huku Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salim Kassim Ali akisema utafiti huo utawahusisha watu wa miaka 15+.

Utafiti huo, unasimamiwa kwa pamoja kati ya Tume ya Ukimwi Zanzibar na Tanzania Bara, Ofisi za Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Serikali ya nchi ya Marekani, na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kwa mara ya kwanza deni la Taifa USA lafikia $31 trilioni
Ruvu Shooting yamuibua Mwamnyeto, aisubiri Al Hilal