Rais William Ruto amewasili nchini Tanzania Jumapili, Oktoba 9, kwa ziara rasmi ya siku mbili ambapo Oktoba 10 Ruto anategemewa kuhutubia watanzania kupitia waandishi wa habari ikiw ani pamoja nakupata nafasi ya kuzungumza na Raisn Samia Suluhu Hassan Ikulu.

Ruto ameandamana na mke wake Rachel Ruto na waziri mteule wa Masuala ya Kigeni Alfred Mutua na walipokelewa na Waziri wa Mambo ya nje na SUhirikiano wa Afrika Mashariki, nchini Tanzania, Dkt. Stergomena Tax.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu anatazamiwa kukutana na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu, katika Ikulu ya Dar es Salaam, ambapo wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya faragha Jumatatu, Oktoba 10.

Rais Ruto atahutubia wanahabari kabla ya kuhudhuria chakula cha mchana katika Ikulu ya Tanzania, kulingana na taarifa ya serikali ya Tanzania.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema Kenya iko makini kupanua fursa ya biashara na jirani yake Tanzania ambayo ni mshirika wa kimkakati katika kanda ya Afrika Mashariki(EAC).

Ziara ya Ruto nchini Tanzania inajiri saa chache baada ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Uganda na katika maadhimisho hayo Ruto alihimiza ushirikiano zaidi wa nchi za Afrika Mashariki, akimuomba Rais Museveni kuongoza hilo.

“Tunaweza kutengeneza ustawi na kuunganisha fursa katika nchi zetu kwa faida ya watu milioni 300 Afrika mashariki na watu bilioni 1.2 katika bara la Afrika, ni nafasi yetu sisi viongozi na wananchi wa ukanda wa Afrika Mashariki tushirikiane ili tuweze kubadilisha mipaka yetu ambayo leo hii imeonekana kuwa vizuizi na kuigeuza kuwa madaraja ili bidhaa, huduma na watu waweze kuvuka Afrika Mashariki bila vikwazo,” alisema Ruto.

Ruto amefanya ziara katika mataifa kadhaa ikiwemo Uingereza alipohudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II, Marekani kuhudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Ethiopia, Uganda na sasa Tanzania.

Dkt. Kikwete atoa neno maonesho Viwanda na Biashara
Ajali ya Boti yauwa 76 eneo la mafuriko