Russia na Iran zimekanusha kuhusu utoaji wowote wa ndege zisizo na rubani kwa Moscow, katika vita vyake nchini Ukraine, wakati Umoja wa Ulaya ukiahidi vikwazo vipya dhidi ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Katika mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, Naibu Balozi wa Urusi, Dmitry Polianski na Balozi wa Iran, Amir Said Iravani wamesema shutuma hizo hazina msingi na kwamba hakuna ushahidi wowote uliotolewa, huku Urusi ikibaini kuwa ndege zisizo na rubani inazotumia, zilitengenezwa na taifa hilo.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Kidiplomasia ya Umoja wa Ulaya, Nabila Massrali amesema umoja huo umekusanya ushahidi wa kutosha, unakionesha kuwa ndege zisizo na rubani zilizotumiwa na Moscow zilitolewa na Tehran, na kwamba Mataifa ya Ulaya yanatayarisha jibu la wazi, la haraka na thabiti.

Oktoba 17, 2022, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky alilaani mashambulizi mapya ya Urusi yaliohusisha makombora na ndege zisizo na rubani zilizopachikwa jina la kamikaze kutokana na kuharibika baada ya kufanya shambulizi, kutaja shambulio hilo kama ni ugaidi dhidi ya raia.

Marekani yajipanga tishio la kuvamiwa na Taiwan
IGP Wambura afanya mabadiliko Jeshi la Polisi