katika mji mkuu wa Ghana, Accra Wafanyabiashara wamefunga maduka na biashara zao ili kushiriki maandamano ya siku tatu kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha, wakati nchi hiyo ya Afrika Magharibi ikipambana na anguko la kiuchumi kutokana na vita vya Ukraine.

Ghana, inakabiliwa na mzigo mkubwa wa deni na mfumuko wa bei katika kiwango cha juu cha kihistoria cha asilimia 37 kwa mwezi Septemba, wakati sarafu ya cedi inayotumika nchini humo ikiwa imeshuka thamani dhidi ya dola ya Marekani.

Muungano wa Wafanyabiashara wa Ghana (GUTA), ulisema hatua hiyo ilituma ishara kwa serikali kwamba wamechanganyikiwa kutokana na usimamizi mbaya wa uchumi.

Wanabainisha kuwa, “Serikali inapaswa kusikiliza maombi ya wafanyabiashara, kwani sekta binafsi ni uti wa mgongo wa uchumi unaoajiri vijana wengi na kwamba kuajiri kijana mmoja au wawili kuuz biashara kunasaidia kuwatoa vijana wasio na kazi mitaani.”

Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo yuko chini ya shinikizo kuhusu usimamizi wake wa uchumi, baada ya kubadili msimamo wake na kuingia katika mazungumzo na IMF kuhusu mkopo wa dola bilioni 3, ili kufadhili fedha za umma.

Hata hivyo, Benki kuu ya Ghana imeongeza kiwango cha mikopo kwa asilimia 10 katika jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei, huku Shirika la Fedha la Kimataifa IMF likianza mazungumzo na Ghana na maafisa wa IMF wakisema wanatarajia kufikia makubaliano kabla ya mwisho wa mwaka huu.

IGP Wambura afanya mabadiliko Jeshi la Polisi
Muundo mpya usimamizi maadili, haki za watumishi