Mkuu wa operesheni za Jeshi la majini la Marekani Michael Gilday, amesema wanapaswa kujiandaa kukabiliana na uwezekano wa uvamizi wa Taiwan mapema kuanzia mwaka huu.

Gilday, ameyasema hayo akiashiria hali ya wasiwasi kuhusu nia ya China kuelekea katika kisiwa hicho, wakati akifanya mazungumzo na shirika la utafiti la Atlantic Council.

Taipei, Taiwan. Picha: Heritage.org

Hata hivyo, Gilday aliulizwa kuhusu hotuba ya rais wa China Xi Jinping wakati wa kongamano la chama cha Kikomunisti siku ya Jumapili na iwapo anakubaliana na matamshi ya mkuu mwingine wa jeshi la Marekani kwamba China iko tayari kuiteka Taiwan kufikia mwaka 2027.

Akijibu hoja hiyo amesema, “Sio tu kile ambacho rais Xi anasema, lakini vile watu wa China wanavyofanya na kuongeza kuwa kile walichokiona katika muda wa miaka 20 iliyopita ni kwamba China imetekeleza kila ahadi iliyotoa mapema kuliko ilivyosema itatekeleza.”

Kenya yazindua basi linalotumia umeme
Urusi yakanusha kutumia ndege zisizo na rubani