Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally amerusha Kijembe katika mitandao ya kijamii, akilenga mchezo wa Jumapili (Oktoba 23), utakaoshuhudia wakicheza dhidi ya Young Africans.

Simba SC itacheza dhidi ya Young Africans siku hiyo, ikiwa na deni la kulipa kisasi cha kupoteza mara mbili mfululizo dhidi ya Mtani wake, ikifungwa 1-0 kwenye mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ msimu uliopita, kisha ikapoteza tena kwa 2-1, katika mchezo wa Ngao ya Jamii mwezi Agosti mwaka huu.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kurusha Kijembe hicho, huku akiweka picha ya Mashabiki wa Simba SC na Young Africans wakiwa pamoja.

Ahmed Ally ameandika: Kwenye kila familia kuna yule mtu asiyekua na malengo yaani yupo yupo tuu.
Kwenye familia yetu ya Tanzania tupo wenye malengo na mipango .

Simba Sports – Makundi ya CAF.

Simba Queens – Makundi CAF.

Serengeti Girls – Robo fainali World Cup.

Ramadhani Brothers Ubingwa wa dunia Sarakasi.

Yupo uyo mmoja sasaa hana malengo yeyote na haoni aibu licha ya kuwa yeye ndo wa kwanza kuzaliwa.

Matrekta yatajwa chanzo cha ajali Barabarani
Hersi Said: Wachezaji wameahidi kurudisha furaha